Mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es Salaam kupitia tiketi ya (CCM) Eugen Mwaiposa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini nyumbani kwake Dodoma.
Kwa mujibu wa Naibu Spika
wa Bunge Mh. Job Ndugai ambaye amelitangazia bunge leo majira ya saa 7 mchana,
marehemu Mwaiposa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda
mrefu.
Ndugai amesema kuwa kwa
sasa msiba upo nyumbani kwake eneo la Chadulu Dodoma ambapo pia familia yake
inasubiria hapo kwa ajili ya kuaga mwili wake shughuli ambayo itafanyika kesho
(Jumatano).
Bunge limeahirishwa hadi
keshokutwa saa 3 Asubuhi.
Mungu ametoa Mungu ametwaa
jina lake lihimidiwe. R.I.P

No comments:
Post a Comment