Wanafunzi sita wa sekondari
ya Makatekista na mkuu wa sekondari hiyo Padri Hyasinti kawonga wamefariki
dunia na wengine ishirini na sita kujeruhiwa kati ya hao wanne hali zao
zikiwa mbaya baada ya gari aina ya Landrover wanten kutumbukia kwenye korongo
na kuwaka moto katika kata ya Kigonsera wilayani Mbinga mkoani
Ruvuma.
ITV
imefika eneo la tukio Kigonsera wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma na kushudia
kijiji cha Kigonsera kikiwa katika hali ya simanzi ambapo mganga mfawidhi wa
kituo cha afya Kigonsera Dkt Patrick Mhagama amesema wamepokea miili saba na
majeruhi ishirini na sita na kwamba miili imeunngua vibaya kiasi cha kushindwa
kutambulika baada ya gari hilo aina ya Landrover wanten kuwaka moto.
Mashuhuda
wa tukio hilo wanasema ajali hiyo ilitokea baada ya kufeli breki na derva
ambaye alikuwa marehemu Padri Hayasinti Kawonga akakata kona ndipo alipoingia
kwenye korongo na ikatokea shoti na gali likawaka moto huku hilo likiwa ni
tukio la tatu katika miaka tofauti kuua watu saba ambapo kuna wanajeshi saba
walikufa kwa ajali ya gari na kufuatiwa na ajali ya maji ilioyoua watoto saba
waliosombwa na maji katika kata ya Kigonsera.
Mwenyekiti
wa kitongoji cha misheni katika kata ya Kigonsera Bw. John Kafarapia amesema ni
pigo kufiwa na padri Kawonga aliyekuwa mkuu wa shule ya sekondari ya
Makatekista na mfadhiri wa wananchi mbalimbali.
PICHA NYINGINE

