1. Ujinga, bila
shaka hii ndio furaha ya watu hawa watangazania wasio na kumbukumbu, hayati
baba wa taifa alipata kusema tunasumbuliwa na maladhi matatu na moja ya maladhi
yale kama ninakumbukumbu ya kuniwezesha kuwa mkweli ni ujinga ambao mpaka baba
wa taifa anapumzika kwa amani alionekana kwa dhati ya moyo wake akipigania
janga la ujinga kwa kuwa katika kipindi chake tuliona na tumehadithiwa namna
watu wa nyakati zake walivyopata elimu kwa raha mpaka kuweza kuwa wanakula
mayai na karanga mashuleni na wengi wao wakisomeshwa bure ili kuja kulisaidia
taifa la tanzania baadae wengine walipelekwa Cuba,Urusi na nchi mbalimbali
ughaibuni ili kuweza kufuta ujinga na kuja kuwakomboa watanzania wakuzamia
wakaishia huko,waliorudi na kutunufaisha tumewaona na wale wenye uelewa kuliko
wengine baada ya kufutwa ujinga wakaona ni bora kutupandikiza ujinga kwa kuweka
mifumo mibovu ya elimu mpaka elimu kuwa biashara,elimu sasa ni gharama kuliko
hata ujinga wenyewe na hata elimu utayoipata baada ya kuinunua kwa gharama ya
juu imekuwa haina msaada kutokana na ukosefu wa ajira,ugumu wa upatikanaji wa
mitaji kwa ajili ya kukiajiri,na hata silabasi isiyomjenga mwanafunzi
kujitegemea zaidi ya dhana ya ajira na kuwa na taifa lililokosa maadili kwa
wale waliobahatika kushikwa mikono na kupata ajira katika ofisi za serikali.
Asilimia kubwa ya watanzania ambao ni fungu la kukosa kwa maana kama
umebahatika kupata kimoja hiki kingine sahau nikiwa na maana umebahatika
kununua elimu sahau ajira.
2. ukosefu wa
elimu, linapokuwa linajadiliwa swala hili huwa napata shida kuelewa kuwa ndani
ya bunge letu la jamhuri ya muungano wa Tanzania huwa linabaadhi ya wabunge
kutoka mataifa mengine au wote ni watanzania kama jina la bunge letu
linavyoitwa, wengi mtajiuliza kwa nini nimechelea kusema hivyo, ati watanzania
kusoma bure haiwezekani kuanzia chekechea/vidudu mpaka elimu ya juu eti kwa
kuwa serikali haina fedha za kutosha kuendesha zoezi hilo, lakini tujiulize ni
kiasi gani kinatakiwa kila mwaka kwa ajili ya wanafunzi wenye vigezo vya kusoma
mpaka ukomo wao kulingana na katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ambayo kwa
kumbukumbu ndogo niliyonayo inasema yampasa mtu yeyote mwenye vigezo vya kusoma
aweze kusoma ama kusomeshwa na serikali na kama atafikia vigezo vya kuajiriwa
pia serikali imfanyie hivyo,sasa wale baadhi ya wabunge na mawaziri walioacha
kuitwa wabunge ambao nina wasiwasi na uraia wao wanaposema serikali haina uwezo
wa kusomesha na kutengeneza ajira wakati huo huo tukirejea kwenye masakata ya
ESCROW,KIGODA,MEREMETA,IPTL,RICHMOND,NBC,MISHAHARA HEWA,BUNGE LA KATIBA LILILOBADILISHA
MAUDHUI YA RASIMU YA KATIBA,MIKATABA INAYOSAINIWA MAHOTELINI,KUSAMEHE
KODI,UTAIFISHAJI WA VIWANDA NA MASHIRIKA YA UMMA PAMOJA NA KUYAFILISI KUTOKANA
NA UTENDAJI MBOVU MFANO RELI YA KATI,TTCL,AIR TANZANIA,URAFIKI,SUNGURA N.K
usishangae kwanini nimeandika kwa herufi kubwa labda herufi ndogo
zisingeonekana vizuri, lakini haya yote ndugu yangu kwao yamewezekana na
yanendelea kuwezekana kwao ila sio kumpeleka mtoto wako shule akapate elimu ya
bure au kufuta ujinga kama walivyofanyiwa wao hawa ambao wengi wao nimeanza
kuutilia shaka uraia wao.
3. Ukosefu wa
matibabu thabiti, hapa unaweza kuandika makala huku unatokwa na machozi ndugu
msomaji yaani hata takwimu kuzifuatilia naogopa kwa sababu haziendani na miaka
hamsini ya uhuru wa nchi yetu. Wahanga wakuu hapa ni wakina mama,wakina mama
wajawazito na watoto. Siku hizi ukienda hospitali hasa hizi hospitali zetu za
umma/serikali utaambulia ushauri na si matibabu, kwasababu unaenda hospitali
ukiwa mgonjwa mahututi kama hauna fedha basi imekula kwako utamwona daktari
atakushauri na kukueleza dalili za ugonjwa ulionao ni ugonjwa gani alafu kauli
ya mwisho itakuwa dawa zinapatikana katika duka fulani mtaa fulani hapa
zimetuishia na wala si kosa la daktari kwani ukienda kwa Msd (medical store
department utaambiwa ni jumla ya kiasi gani wanaidai serikali) kwa kweli
inasiitisha ikiwa wakati huo huo kuna baadhi ya watanzania wenzetu wanakatwa
fedha kwa minajiri ya kuwa na bima za afya zao lakini wanavyokutana navyo
hospitali si vya kusimulia.vijijini kilio hiki ni kikubwa zaidi kwani hupelekea
watu hata kufa/kujifungulia njiani kutokana na kukosa hospitali au zahanati
karibu na makazi sawa Tanzania ni nchi ya Amani na Upendo je upo wapi Upendo na
Amani kwa watoto vichanga na mama zao wanao fariki njiani kabla ya kufika
hospitali ama zahanati???! Jamani watangaza nia tuwe na huruma mliyotufanyia
yanatosha na sasa ni wakati wa kuwapa wengine vijiti mtatumaliza sasa sijui
mtatawala viumbe gani kama watanzania wanaisha kwa Malaria,kifua
kikuu,ukimwi,kipindupindu,saratani,kisukari,presha na hasa kuwapoteza malaika
ambao ni kizazi cha kesho wakati wa kujifungua.
4. Ukosefu miundombinu
imara na thabiti,hapa ndipo serikali inapoanzia kuwa serikali ya historia
tumejenga barabara kilimita 1000,mara kilomita 7000 sawa tumekubali je baada ya
kujenga kilimita zote hizo mbona foleni kwenyi miji hazipungui,mazao kutoka
mashambani yameendelea kuwa juu kutokana na gharama za usafirishaji,watanzania
wamekua wakipungua kila siku kutokana na ajali za mabarabarani ukiuliza sababu
dereva alikuwa akikwepa shimo la barabara iliyopitishwa bajeti yake mwaka juzi
wakati wenzetu wana barabara zina umri wa uhuru wetu na hazina mashimo haya
yote watangaza nia ni mazao ya chama chenu na uongozi wenu sasa napata wakati
mgumu mnaposema nyinyi wenyewe mtafanya tofauti na mlivyokuwa mkifanya awali.
Kwa lugha nyepesi kauli na hotuba zenu ni nzuri hasa mngekuwa mnatokea upande
wa pili wa shilingi,ila kwa staili hii ya kuvaa ngozi ya kondoo ndani chui kwa
kweli kauli zenu hazina mashiko katika serikali ya kichwa changu mpaka pale
hata mmoja wenu akaweza kunieleza vizuri nimuelewe alikuwa wapi wakati wenzake
wakifanya kazi kwa umoja kutufikisha hapa tulipo maana kidole kimoja hakivunji
chawa.
5. kuongezeka
kwa gharama za maisha wakati kipato ni kidogo
6. ongezeko
kubwa la aliyenacho na asiyekuwa nacho
7. ufisadi/matumizi mabaya ya madaraka, nukuu”
waziri wa kilimo na ushirika,Wasira
amesema ndani ya ccm hakuna mafisadi bali neno fisadi ni msamiati
unaotumiwa na wapinzani kama njia ya kuwakashifu makada wa chama tawala. Wasira
alitoa kauli hiyo wakati alipotakiwa na waandishi wa habari kueleza namna
atakavyopambana na mafisadi ikiwa atapata fursa ya kuliongoza Taifa. Wasira
alibainisha kuwa katika mijadala mbalimbali swali la ufisadi halipaswi
kulizungumza kwa kuwalenga watu na badala yake linapaswa kujadiliwa kama hoja
na kutafutiwa ufumbuzi kama ilivyo swala la umaskini na uwajibikaji.
“ninavyofahamu mimi ndani ya ccm hakuna mafisadi,lakini kama hoja ufisadi
sitaifumbia macho,nitazungumza na kuishughulikia”, alisema Wasira. Kweli ama si
kweli kwa lugha nyingine ni uongo ama si uongo ninatumaini jibu unalo wewe
mtanzania katika serikali ya kichwa chako kazi kumkichwa
8. ukosefu wa
ajira kwa vijana na mifumo ya uwekezaji mzuri wa akiba uzeeni kwa wariojiajiri
na kukosa ajira.
Na kuondoa dhana ya demokrasia ya utawala wa
watu kwa ajili ya watu na unao tawaliwa na watu kwa sababu binadanu wa kawaida
ukimpatia majanga kumi kama tulivyoyaorodhesha hawezi kuishi kama binadamu ni
lazima atakengeuka na kuwa kiumbe wa aina nyingine ali aweze kupata maslahi
yake kama binadamu na hapa ndipo tunawapata wadai haki na wanaobatizwa majina
ya waasi.
Makala hii
imeandaliwa na
Godlove
Malele
p.o.box 7583
Dsm
godlovemalele@yahoo.com

No comments:
Post a Comment