Designer Hebron Malele More information *Phone number 0659-994437*: hebronjohana@yahoo.com!!  NICE FOR ALL :

Saturday, 6 June 2015

#‎MICHEZO‬ SERENA ATWAA TAJI LA FRENCH OPEN.



Mchezaji namba moja kwa ubora katika tennis duniani Serena Williams ametwaa taji la 20 la Grand Slam katika michuano ya wazi ya ufaransa (French Open) baada ya kumfunga Lucie Safarova kwa jumla ya seti 2-1.
Katika mchezo wa fainali uliopigwa leo na kudumu kwa takriban saa 2 na dakika 1, Serena amemshinda Safarova raia wa Czech anayeshikilia nafasi ya 13 katika ubora wa dunia kwa seti 6-3 6-7, 6-2.
Kwa ushindi huu Serena anakuwa ni mcheza tennis wa tatu kushinda mataji 20 ya Grand slam (kwa mchezaji mmoja mmoja) ambapo wengine ni mjerumani Steffi Graf na raia wa Australia Margaret Court kati ya mwaka 1960 na 1973.

No comments:

Post a Comment