Designer Hebron Malele More information *Phone number 0659-994437*: hebronjohana@yahoo.com!!  NICE FOR ALL :

Monday, 22 June 2015

YALIYOJILI:Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limemteua Sheikh Aboubakar Zuberi kuwa Mufti Mpya wa muda.



Baraza Kuu La Waislamu Tanzania (BAKWATA), leo saa Tano asubuhi linatarajia kutangaza jina la Kiongozi Mkuu wa Waislamu Tanzania (MUFTI).

Nafasi ya Mufti ilikuwa wazi baada ya Kifo cha Mufti Issa Bin Shaaban Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15, 2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Hatimaye atakayekaimu nafasi ya Mufti Mkuu wa Waislamu nchini Tanzania amepatikana!

Aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa baraza kuu la Ulamaa BAKWATA, Sheikh Abubakar Zuberi, ndiye aliyetajwa kushika kwa muda wa siku 90 nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Waislamu Tanzania (MUFTI) kufuatia kifo cha aliyekuwa Mufti Mkuu, Sheikh Idd Shaaban Simba aliyefariki mnamo wiki moja iliyopita, kabla ya uchaguzi utakaofanyika kumpata kiongozi mkuu kwa mujibu wa taratibu za kiislamu.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanaotajwa kuweza kushika nafasi hiyo ni pamoja na Kadhi Mkuu, Sheikh Abdallah Mnyasi na Sheikh Ali Muhidin Mkoyogile.

Wengine ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Ferej, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Kiburwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Hamid Masoud Jongo.

Sheikh Abubakar Zuber ametangazwa asubuhi hii ya leo kuwa ndiye mkaimu wa nafasi hiyo ya juu kabisa kiuongozi katika dini ya kiislamu.

Sheikh Zuber atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (siku 90) kuelekea katika uchaguzi wa kumpata atakayerithi nafasi hiyo kwa mamlaka kamili.

Zipo hisia pia kuwa huenda Sheikh Abubakar akapitishwa kuishikilia nafasi hiyo baada ya kipindi hicho kupita endapo kura nyingi zitaelekezwa kwake!

No comments:

Post a Comment