Chelsea
wamemsajili Radamel Falcao, 29 kutoka Monaco, na wanatarajia kutangaza mkataba
wake wiki ijayo (Daily Star), mshambuliaji wa Manchester United Robin van
Persie anasisitiza kuwa anataka kubakia Old Trafford licha ya taarifa kuwa
huenda akaondoka (Daily Mirror), Manchester City ambao wamehusishwa na Raheem
Sterling, Paul Pogba na Kevin De Bruyne wataendelea na usajili licha ya
wasiwasi wa kuchukuliwa hatua na Uefa kuhusiana na sheria za kifedha za uhamisho (Manchester Evening News)
Manchester United wanapanga kutoa pauni milioni 30 kumchukua kiungo
mshambuliaji Filipe Anderson, 22 kutoka Lazio (Sun), Man Utd pia inaweza
kumsajili kipa wa Ajax Jasper Cillissen, 26, kuziba pengo la David De Gea, 24,
ambaye anahusishwa kwenda Real Madrid (Daily Telegraph), mashambuliaji wa
Sevilla, Carlos Bacca, 28, ambaye anaripotiwa kutakiwa na Man Utd na Arsenal,
anataka kwenda Roma ya Italia (Daily Mail), West Ham wanatka kumsajili
mshambuliaji wa QPR Charlie Austin, 25. Mchezaji huyo anawindwa na Southampton
na Newcastle United (London Evening Standard), Everton wanafikiria kumchukua
mshambuliaji wa Arsenal Lucas Podolski , 29 ambaye amecheza kwa mkopo Inter
Milan msimu uliopita (Daily Star), mshambuliaji kutoka Croatia anayechezea
Atletico Madrid Mario Mandzukic, 29, huenda akachukuliwa na Wolfsburg, iwapo
Bas Dost, 26 ataondoka Ujerumani na kwenda Newcastle. Mandzukic pia ananyatiwa
na Liverpool na Manchester United (AS), kiungo wa Arsenal Mesut Ozil amesema
wachezaji wenzake wa Ujerumani Mats Hummels na Benedikt Howedes wana viwango
vya kuwika Uingereza. Hummels, 26, amehusishwa na kuhamia Man Utd, huku taarifa
zikidai kuwa Howedes, 27, ananyatiwa na Arsenal (Guardian) meneja wa Chelsea
Jose Mourinho anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya
pauni milioni 30 kwa mwaka kusalia Stamford Bridge (Daily Mail). Uhamisho
uliothibitishwa nitakujulisha ukithibitishwa. Tetesi nyinine kesho tukijaaliwa.

No comments:
Post a Comment