Designer Hebron Malele More information *Phone number 0659-994437*: hebronjohana@yahoo.com!!  NICE FOR ALL :

Wednesday, 24 June 2015

YALIYOJILI:Mfanyabiashara aitwae Mathias Manga wa Jijini Arusha amepigwa risasi ya mgongoni.






Habari zilizojili muda huu ni kwamba Mathias Manga, bilionea wa jiji la Arusha, na Diwani wa Kata ya Mlangarini Arumeru Magharibi (CCM), amepigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akielekea nyumbani.

Imeelezwa kuwa watu hao walifanya jitihada zote lengo ilikuwa ni kumteka lakini mfanyabiashara huyo alijitetea mpaka akajitoa ndio wakaamua kumpiga risasi.


Amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Selian iliyopo mkoani humo, Waandishi wa habari waliopo Arusha ambao wamezuiwa kuingia katika chumba alicholazwa wamesema amepigwa risasi katika eneo la Mgongoni (Hajaumia sana).

No comments:

Post a Comment