Designer Hebron Malele More information *Phone number 0659-994437*: hebronjohana@yahoo.com!!  NICE FOR ALL :

Thursday, 25 June 2015

YALIYOJILI:Vyuo vitatu vya futwa na serikali.




Baraza la Elimu la Ufundi (Nacte) limefuta usajili wa vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vingine 16 kutokana na kukiuka masharti ya usajili.
Vyuo vilivyofutiwa usajili ni Dar es Salaam College of Clinical Medicine, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences, vinavyohusika na elimu ya tiba, na Institute for Information Technology kinachofundisha elimu ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama).
Akitangaza uamuzi huo jijini hapa jana, kaimu katibu mtendaji wa Nacte, Dk Adolf Rutayuga alisema vyuo hivyo vimeshindwa kurekebisha kasoro ambazo baraza hilo lilizibaini na kuvitaka kufanya marekebisho. Alisema baraza hilo lilitoa notisi ya siku 30 likivitaka vyuo vyenye upungufu katika usajili na ithibati kutoa maelezo na kufanya marekebisho.
Kaimu mkurugenzi huyo alisema baadhi ya vyuo vilifanya marekebisho kama vilivyoogizwa.
Alitaja makosa yaliyokiukwa kuwa ni kumalizika kwa muda wa usajili, kutoanza mchakato wa kupata uthibitisho wa kufikia viwango vilivyowekwa, kumalizika muda wa ithibati na kutoomba upya usajili pamoja na vyuo kuamua kusitisha mafunzo.
Alisema mbali na vyuo hivyo vitatu vilivyofutiwa usajili, vingine 16 vimezuiwa kusajili wanafunzi au kushushwa hadhi.
Alisema Darmiki College of Educational Studies imezuiwa kusajili wanafunzi baada ya kubainiki kinadahili bila kusajiliwa.
Alivitaja vyuo vilivyoshushwa hadhi kuwa ni Sura Technologies, Institute of Management and Information Technology, Techno Brain, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi, Mbozi School of Nursing, KCMC AMO Ophthalmology School, KCMC AMO Anaesthesia School, Advanced Pediatrics Nursing KCMC.
Vingine ni AMO Training Centre cha Tanga, CATC Sumbawanga, CATC Songea, COTC Maswa, COTC Musoma, Dental Therapists Training Center, Ngudu School of Environmental Health Sciences Kwimba na KCMC AMO General School Moshi.

HOT NEWS: Mtoto auawa kikatili Dar.




Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka mitano hadi sita ameuwa kikatili jijini Dar es salaam baada ya kubakwa na kasha kunyongwa shingo huku akidaiw akunyofolewa sehemu za siri.
Mwili wa mototo huyo unadaiwa kutelekezwa katika moja ya nyumba iliyokuwa haijaisha na kugunduliwa na kijana aliyekuwa akiokota chupa tupu za maji eneo la tabata kisiwani, Dar es salaam.
Baadhi ya mashuhuda walisema  walilaani tukio hilona kusema na ukatili  huo ni wa kwanza kutokeo mtaani hapo.

Angalia video mpya ya Kcee ft Davido inayoitwa 'Ogaranya'.


Wednesday, 24 June 2015

YALIYOJILI:Marijan Abubakar, maarufu kama 'Papa Msoffe' aliyekuwa mahabusu kwa kesi ya mauaji ya kukusudia, ameshinda mashtaka ya mauaji, amebakiwa na kesi ya kughushi nyaraka.




Taarifa zinaeleza kuwa Papaa Msoffe Chuma cha reli hatimae amerudi uraiani baada ya mashtaka ya mauaji kubadilishwa na kuwa shtaka la kugushi hivyo anaweza kupata dhamana.

Angalia video mpya ya Davido ft Meekmill inaitwa Fansmi.


YALIYOJILI:Mfanyabiashara aitwae Mathias Manga wa Jijini Arusha amepigwa risasi ya mgongoni.






Habari zilizojili muda huu ni kwamba Mathias Manga, bilionea wa jiji la Arusha, na Diwani wa Kata ya Mlangarini Arumeru Magharibi (CCM), amepigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akielekea nyumbani.

Imeelezwa kuwa watu hao walifanya jitihada zote lengo ilikuwa ni kumteka lakini mfanyabiashara huyo alijitetea mpaka akajitoa ndio wakaamua kumpiga risasi.


Amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Selian iliyopo mkoani humo, Waandishi wa habari waliopo Arusha ambao wamezuiwa kuingia katika chumba alicholazwa wamesema amepigwa risasi katika eneo la Mgongoni (Hajaumia sana).