Rapa Proffesa Jay amewakahikishia mashabiki wake kuwa endapo hesabu zitaenda sivyo na akakosa kiti cha ubunge anachowania kwa sasa, atarejea kwa nguvu zote katika muziki ambao umekuwa ndiyo msingi wa shughuli zake.
Jay, akiwa na historia kubwa katika sanaa ya muziki Tanzania, amekoleza kuwa, kufanikiwa kwake kuchukua nafasi hiyo vilevile hakutamfanya kuacha muziki, na ataendelea kuuwakilisha kutokana na mchango mkubwa wa tasnia hiyo katika maisha yake.

No comments:
Post a Comment