Mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Eldoforce Bilohe jana alitinga makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kuteuliwa kuwa mgombea urais, bila kuwa na ada huku akiwa amebeba maji ya chupa kwapani.
Bilohe ambaye alisema elimu yake ni ya darasa la Saba, aliwasili makao makuu ya CCM muda wa saa 5:40 asubuhi na kuelekea Ofisi ya kupokea wagombea ndani ya ofisi baada ya kuwapita waandishi wa habari wakiwemo wapiga picha, waliokuwa wamejipanga kumsubiria, lakini aliwapita waandishi bila kumtambua kuwa ni mgombea.

No comments:
Post a Comment