Makala
“ Hakuna mtu aliye na kumbukumbu za kutosha
kumwezesha kuwa muongo”
Abraham lincoln (1809-1865)
Baada
ya kumsoma mwanafalsafa huyu na falsafa zake mbalimbali kwa leo nimetokea kuvutiwa
na falsafa hii hasa kutokana na kipindi kigumu tulichopo kwa wakati huu wa
kuelekea uchaguzi mkuu ambapo kila mwanasiasa anataka kuwafanya watanzania ni
kichwa cha mwendawazimu kama ambavyo alipata kuzungumza miaka fulani mzee wa
ruksa na raisi mstaafu wa awamu ya ya pili Ndugu, Ali Hassan Mwinyi.
Ni
kwaninini natokea kuvutiwa na mwanafalsafa huyu wa kutokea ughaibuni aliyepata
kuishi mwanzoni mwa miaka ya 1800, hili naweza kuliweka wazi ni kwakuwa
viongozi wetu wengi wa sasa ambao wanajibatiza au tumewabatiza majina mapya ya
watangaza nia ya kuwania uraisi kupitia chama cha mapinduzi ccm wanasadifu kwa
hali ya juu kabisa kauli hii iliyowahi kuzungumzwa na mwanafalsafa aliyewahi
kuwa raisi wa taifa kubwa la marekani akikumbukwa kuwa mmoja ya mwasisi mkubwa
wa demokrasiahasa baada yakutoa ile
kauli maarufu ya “democracy is
the government of the people for the people by the people” kwa lugha yetu hadhimu ya kiswahili
angelisema” demokrasia ni utawala wa
watu kwa ajili ya watu unao tawaliwa na watu”
Tukirejea
muongozo wa makala yetu,” hakuna mtu aliye na kumbukumbu za kutosha kumwezesha
kuwa muongo” nashawishika kabisa kusema uongo ni dhambi tena kuifanya kwa
makusudi na kuirudia rudia inaweza ikawa ni dhambi isiyosamehewa kabisa na
wananchi ambao ndio wahanga wakuu wa maisha magumu yanayoambatana na
1. njaa,
2. Umaskini,
nukuu kutoka kwa mmoja ya watangaza nia “nachukia
sana umaskini”,na kuuchukia kwake umaskini ndio kumemfanya awaze kutangaza
nia ya kugombea uraisi na mtu huyu amekuwako serikali tena katika nyadhifa za
juu kabisa kwa zaidi ya awamu nne{4} za miaka mitano mitano akiwa anaingia
kwenye baadhi ya vikao vya baraza la mawaziri na akiwa ameshawahi kuwa mmoja ya
watu wa juu kabisa katika ngazi ya chama kwa ajili ya kutengeneza sera za chama
chake na kuwa kampeni meneja wa raisi anayeenda kumaliza majukumu yake hivi
karibuni tena akisimama na kujinadi mbele ya wananchi jinsi alivyoweza
kuyatimiza baadhi ya majukumu yake hayo katika kipindi kilichopita…hapo ndipo
ninapo jiuliza kutokana na jinsi anavyouchukia umaskini mpaka kumpelekea kuwa
mmoja ya watangazania ni kwanini asingeweza kutumia nguvu na ushawishi wake wa
mafuriko yasisyoweza kuzuiliwa kwa mkono kuweza kupiga vita umaskini kwa
kipindi chote alichokuwa akihodhi madaraka na nafasi za juu ndani ya chama
chake na serikali Ama kweli Abraham Lincoln have never died he just passed away
(kwa lugha yangu tamu na nzuri ya kiswahili ni kwamba Abraham Lincoln hakufa
bali amepita kama njia hii ni kutokana na kwamba maneno mengi yaliyowahi
kuzungumzwa na watu wa kariba yake yameendelea kuishi, hakuna mtu aliye na
kumbukumbu za kutosha kumwezesha kuwa muongo. Miaka ishirini{20} ni sawa na
awamu nne{4} za miaka mitano mitano{5},pia ni sawa na miaka ishirini ya kijana
mpiga kura halali wa kitanzania ambae alizaliwa wakati watangaza nia wengi
wakianza kuitumikia serikali katika nyadhifa za uwaziri,ubunge na nafasi
mbalimbali ndani ya chama chao,na wameendelea kuwa huko mpaka sasa je ni kweli
watu hawa wanauchukia umaskini kiasi cha kuwashawishi vijana hawa waliokulia
katika majanga kumi tuliyoyataja hapo juu wanaweza kuwashawishi vijana hawa
ambao ni 60% ya idadi ya watanzania,kwa kweli mjifunze kusoma alama za nyakati
nafikiri vijana wezangu,wakina mama na wazee tunahitaji mabadiliko ya kweli.
Makala hii inaendele siku nyingine endelea kufatilia page hii ya *SAHARA SUPER GYM*
Makala hii
imeandaliwa na
Godlove
Malele
p.o.box 7583
Dsm
godlovemalele@yahoo.com

No comments:
Post a Comment