Chelsea
huenda wakacheza mechi zao za nyumbani ugenini kwa angalau misimu miwili kama
sehemu ya kuongeza idadi ya watazamaji kufikia 60,000 Stamford Bridge
(Guardian), maneja wa Juventus Massimiliano Allegri amesema itakuwa vigumu
kukataa kama dau la maana litatolewa kwa kiungo Paul Pogba. Pogba, 22,
amehusishwa na Chelsea, Manchester United na Manchester City (Gazzetta dello
Sport) Manchester United wamewaambia Real Madrid kuwa hawatafikiria dau lolote chini ya pauni milioni 25 kumnunua kipa
David De Gea (Sun) mshambuliaji Harry Kane, 21, ameshauriwa na Fabrice Muamba
kuwapuuza Man Utd na kubakia Tottenham (Express), Monaco wanawataka kwa mkopo
kungo wa Chelsea Mario Pasalic, 20 na Charly Musonda, 18, kama sehemu ya
mkataba wa Chelsea kumchukua Radamel Falcao kwa mkopo (Telegraph), kocha wa
makipa wa Chelsea anaamini kuwa Petr Cech, 33, anataka kwenda Arsenal (Mirror),
Liverpool wataongeza dau lao kutaka kumsajili beki wa kulia wa Southampton
Nathaniel Clyne baada ya pauni milioni 10 kukataliwa (Liverpool Echo), wakala
wa Roberto Firmino amesema mchezaji huyo wa Hoffenheim ambaye amehusishwa na
kuhamia Manchester United, amethibitisha kuwa mchezaji huyo anataka kuhamia
Uingereza lakini mkataba wowote utafikiwa baada ya michuano ya Copa America
(Bild), Man Utd lazima walipe pauni milioni 35 kama wanataka kumsajili beki wa
Valencia Nicolas Otamendi, 27 (Mirror), Everton wanakaribia kukamilisha usajili
wa winga wa Barcelona Gerrard Deulofeu (Star), Liverpool huenda wakamsajili
beki wa Charlton Joe Gomez, 18 kuziba nafasi ya Sebastian Coates ambaye
anatarajiwa kwenda Sunderland (Guardian), Tottenham wanakaribia kumsajili beki
Kieran Trippier, 21, kutoka Burnley. Liverpool, Newcastle, West Ham,
Bournemouth na Southampton pia wanamtaka (Mail), Spurs pia wanataka kumsajili
Mohamed Salah, 23, kutoka Chelsea (Evening Standard), Inter Milan wameanza tena
mazungumzo na wawakilishi wa Stevan Jovetic na wana uhakika wa kukamilisha
mkataba huo kutoka Manchester City.
PICHA ZAIDI




No comments:
Post a Comment