Manchester
United wanamtaka mshambuliaji wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic, 29, mwaka
mmoja tu baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Spain akitokea Bayern Munich kwa
pauni milioni 18.5 (Sun), United pia wanamtaka beki wa kulia wa Paris St
Germain Gregory van der Wiel, 27, baada ya Dani Alves kuamua kubakia Nou Camp
(Mail), Louis van Gaal pia anafikiria kumfuatilia beki wa kulia wa Southampton
Nathaniel Clyne, 24 (Express), meneja mpya wa West
Ham Slaven Bilic amekabidhiwa fungu la kutosha la kumnunua mshambuliaji wa
Chelsea Loic Remy, 28, na kiungo wa Barcelona Alen Halilovic, 18 (Guardian),
usajili wa kwanza chini ya Bilic utakuwa kiungo kutoka Sampdoria Pedro Obiang,
23, kwa pauni milioni 4.4 (Mail), meneja mpya wa Derby County Paul Clement
anataka kumsajili mshambuliaji wa Hull City Tom Ince, 23, kwa pauni milioni 6
(Mirror), meneja wa Everton Roberto Martinez anataka kumsajili beki wa Crystal
Palace Scott Dann, 28 (Independent), kiungo wa Paris St-Germain Yohan Cabaye,
29, anafikiria kujiunga na Crystal Palace (Le Parisien), meneja wa Tottenham
Mauricio Pochettino anamtaka mshambuliaji Timo Werner, 19 kutoka Stuttgart
(Mirror), mshambuliaji wa Manchester City Alvaro Negredo, 29 atasaini kwenda
Valencia kwa mkataba wa kudumu (Manchester Evening News), Manchester City wapo
tayari kumuuza Edin Dzeko, 29, lakini wanataka pauni milioni 20. Liverpool
hawamtaki tena Dzeko lakini Jose Mourinho anafurahishwa na mchezaji huyo (Daily
Mail), Arsene Wenger anamfuatilia kipa wa Real Madrid, Iker Casillas. Wenger
angependa kumchukua Petr Cech, lakini atamchukua Casillas iwapo atataka
kuondoka Bernabeu (Evening Standard), Real Madrid wanataka kumsajili kipa wa
Espanyol, Kiko Casilla, kuwa kipa msaidizi wa David De Gea (Daily Mirror), PSG
watatazama uwezekano wa kuziba pengo la Zlatan Ibrahimovic kwa kumchukua
Ronaldo msimu ujao baada ya huu mpya (Daily Mirror), Juventus wapo tayari kutoa
pauni milioni 30 kumsajili Oscar kutoka Chelsea, ili kuziba nafasi ya Andre
Pirlo (The Sun), PSG hawatomuuza Marco Verratti msimu huu licha ya kunyatiwa na
Arsenal, Manchester United na Real Madrid (Daily Express), Atletico Madrid
wanakaribia kumsajili mshabuliaji wa Villareal Luciano Vietto (AS), kipa wa
Chelsea Petr Cech anataka kwenda Arsenal. PSG walikuwa wakimtaka, lakini
wamejitoa kwa sababu Cech anataka kubakia London (The Independent), na AC Milan
wamejiunga katika mbio za kumsajili beki wa Atletico Madrid Miranda ambaye
anasakwa pia na Chelsea na Manchester United (Daily Star). Share tetesi hizi na
wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema Cheers!
PICHA ZAIDI




No comments:
Post a Comment