Iker
Casillas amekubali kuondoka Real Madrid na nafasi yake itachukuliwa na David De
Gea, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la taifa la Spain-
Television Espanola. Nahodha huyo wa Real Madrid bado ana miaka miwili katika
mkataba wake Santiago Bernabeu, na kwa mujibu wa taarifa hizo, aliambiwa na
Real Madrid kuhusu nia ya kusajili kipa mwingine msimu huu. Madrid wanatarajiwa
kwa kiasi kikubwa kukamilisha uhamisho wa David De Gea kutoka Manchester
United. Wakati Casillas, 34, akisema mara kwa mara kuwa angependa kumaliza
mkataba wake, lakini pia yuko tayari kuondoka. Television Espanola imesema karibu
vilabu kumi vimeonesha nia ya kumsajili Casillas.


No comments:
Post a Comment