Kiungo wa
Chile Arturo Vidal ameachiliwa na polisi baada ya kukamatwa kwa kosa la
kusababisha ajali kwa madai wa ulevi. Vidal, 28, ambaye ndio anayeongoza kwa
kufunga magoli katika michuano ya Copa America 2015 nchini mwake, Chile,
alipata ajali na Ferrari yake usiku wa Jumanne. Leseni ya kuendesha gari ya
Vidal aliyepata majeraha madogo, imesitishwa, lakini ataendelea kichezea Chile.
"Nimewaangusha watu wote," amesema Vidal akibubujikwa na machozi
baada ya kuachiliwa.

No comments:
Post a Comment