Mshambuliaji
nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi anakaribia kuburuzwa mahakamani
kujibu mashtaka ya kukwepa kulipa kodi, baada ya mahakama ya juu ya Spain
kutupilia mbali rufaa yake. Messi na baba yake, Jorge, wanatuhumiwa kutolipa
kodi ya zaidi ya dola milioni 5 kwa mamlaka za Hispania. Mahakama kuu ilisema
Messi asipewe kinga kwa kisingizio cha kutofahamu yaliyokuwa yakiendelea
kuhusiana na masuala ya fedha zake. Wawili hao, ambao wanakana mashtaka,
wanatuhumiwa kufanya tukio hilo kati ya mwka 2007 na 2009.

No comments:
Post a Comment