Meneja wa
Manchester City Manuel Pellegrini ameahidiwa kupewa fedha za kupindukia ili
kuibadili kabisa timu hiyo iweze kutawala Ulaya (Sun), Pellegrini anataka
kumsajili kiungo wa Juventus kutoka Ufaransa, Paul Pogba, 22, na pia
mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, 20 (Daily Mail), mshambuliaji wa
Real Madrid Karim Benzima, 27, huenda akajiunga na Manchester United katika
uhamisho utakaoshuhudia kipa David De Gea kuondoka Old Trafford kwenda Bernabeu (Telegraph), Arsenal watajaribu
kumnunua kipa Iker Casillas, 34, iwapo Real watakamilisha usajili wa David De
Gea (London Evening Standard), Abou Diaby, 29, huenda akapewa nafasi ya
kuendelea kusalia Arsenal kwa mkataba wa 'kulipwa-kwa-kucheza' licha ya kutajwa
katika orodha ya wachezaji walioachwa (Times), kiungo wa zamani wa Chelsea
Kevin De Bryne, 23, huenda akarejea England baada ya mchezaji huyo wa kimataifa
wa Ubelgiji kuthibitisha kuwa wakala wake amekuwa na mazungumzo na Manchester
City (Sky Sports), meneja wa Chelsea Jose Mourinho amepigwa marufuku kuendesha
gari kwa miezi sita baada ya kukamatwa akiendesha gari kwa kasi ya maili 60 kwa
saa kwenye eneo la maili 50 kwa saa (Mirror), Chelsea wamejaribu kuwakatisha
tamaa wanaomtaka kipa Thibault Courtois, 23, kwa kumuwekea bei ya pauni milioni
73 (Telegraph), beki wa kulia wa England Glen Johnson, 30, anatarajiwa kujiunga
na Besitkas ya Uturuki baada ya kuruhusiwa kuondoka na Liverpool (Liverpool
Echo), Manchester City watamruhusu Micah Richards, 26, kuondoka lakini watabaki
na kipa Richard Wright, 37 ambaye hajacheza mechi hata moja tangu alipojiunga
nao mwaka 2012 (Manchester Evening News), Tottenham wanataka kumsajili beki wa
kulia wa Burnley Kieran Trippier ambaye amehusishwa na Liverpool na Southampton
(Mirror), Inter Milan wanataka kumsajili Javier Hernandez ambaye amerejea
Manchester United baada ya kucheza kwa mkopo Real Madrid msimu uliopita. United
wanataka euro milioni 15 kwa Chicharito (Tuttosport), Real Madrid watatoa dau
rasmi kumtaka David De Gea wiki hii, lakini Manchester United watataka
kumchukua Karim Benzima kama sehemu ya uhamisho huo. Louis van Gaal pia
anamtaka kipa wa Chelsea Petr Cech (Daily Telegraph), Barcelona hawataki tena
kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan kwa sababu anataka
mshahara mkubwa wa euro milioni 10 kwa mwaka (Bild), Everton wanataka kumsajili
mshambuliaji wa Marseille Dimitri Payet (The Guardian), Roma wameonesha dalili
za kumtaka mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku (Daily Mail), Southampton
wanapanga kutafuta kiungo wa kuchukua nafasi ya Morgan Schneiderlin anayedhaniwa
kuelekea Old Trafford. Dau lao la pauni milioni 12 kumtaka kiungo Grzegorz
Krychowiak limekataliwa (Daily Express). Uhamisho uliothibitishwa nitakujulisha
ukithibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

No comments:
Post a Comment