Watu wasiofahamika
wamevamia ofisi mpya ya chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Tawi la
Mburahati kwa madoto na kubomoa ofisi hiyo bila ya kutoa taarifa yoyote kwa
uongozi wa ofisi hiyo.
ITV
imefika eneo la Mburahati kwa madoto zilipo ofisi hizo za Chadema na kukuta
upande wa mbele wa ofisi hiyon ukiwa umebomolewa na baadhi ya vitu
kuvunjwa huku uongozi wa ofisi hiyo ya Chadema ukielekezea lawama kwa
serikali ya mtaa wa Mburahati kwa madoto kwa kuhusika na ubomoaji huo pasipo
kufuata taratibu za ubomoaji.
Akijibu
tuhuma hizo afisa mtendaji wa kata hiyo ya Mburahati hiyo Bi.Scholastica
Matinde amesema sheria hairuhusu kwa chama chochote cha siasa kuweka ofisi
kwenye maeneo ya masoko kama ambayo chama hicho cha Chadema kilivyofanya.
PICHA NYINGINE YA TUKIO


No comments:
New comments are not allowed.